Maswali yaulizwayo kuhusu Opus Dei, Sehemu ya pili (Toleo jipya)

Kwa ajili ya ndugu na dada zetu katika Afrika Mashariki ambao wamekuwa wakitamani sana maandishi na rasilimali katika lugha ya Kiswahili, tunawatolea sehemu ya pili ya makala fupi inayoeleza Opus Dei. Rasimu hii ya kipeperushi imetafsiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na Dk. Walter M.Mbunda.

Photo by Towfiqu barbhuiya on Unsplash.jpg

Je, Mapadre wanaweza kujiunga na Opus Dei?

Mapadre (wasio Watawa) ambao tayari wamepewa daraja la upadre katika Dayosisi hawawezi kujiunga na Opus Dei, lakini wanaweza kuwa sehemu ya Chama Cha Kipadre cha Msalaba Mtakatifu [Priestly Society of the Holy Cross], ambacho kimeungana na ‘Prelature’. Ushirikishwaji wao katika Chama cha Kipadre [Priestly Society] wa Msalaba Mtakatifu hauathiri ushiriki wao katika Dayosisi zao. Wanabaki kuwa mapadre wa Dayosisi, chini ya Askofu kama walivyokuwa awali. Wanaahidi kufuata utakatifu wanapotekeleza majukumu yao ya kipadre, kulingana na mtazamo wa Opus Dei, na wanajitahidi kwa namna ya pekee kuungana na Askofu wao na Mapadre wenzao.

Je wanawake na wanaume wana hadhi sawa katika Opus Dei?

Wanawake na wanaume wanapata hadhi sawa kama watoto wa Mungu na wanaitwa kwa usawa kuiishi imani yao. Wanaume na wanawake wanaoamini Prelature huwa na lengo/nia moja, hutangaza utume [apostolates] unaofanana, wana vipawa na wanafanya kazi katika fani zote zinazoheshimika, na wito sawa wa kujaribu kutakatifuza kazi na maisha ya familia. Aidha, wanawake na wanaume walei wanatekeleza majukumu ya serikali yanayofanana na utume [formation] katika Prelature.

Washirika [cooperators] ni nani?

Opus Dei ina washirika [cooperators] ambao ni Wakatoliki, Wa-Orthodox, Waprotestanti au waumini wa Madhehebu mengine ya Kikristo; Wayahudi, Waislamu, au waumini wa madhehebu mengine; na watu wasio na dini yoyote. Kwa kupitia sala na maombezi yao, kazi na michango/misaada, Washirika husaidia utekelezaji wa shughuli za elimu na kijamii zinazoendeshwa na waumini wa Prelature duniani kote. Mtu hawezi kuwa mwanachama wa Opus Dei kwa kuwa tu alikuwa Cooperator.

Kazi gani za Kitume inafanya Opus Dei?

Neno utume linatafsiriwa kuwa ni juhudi ambazo Wakristo wanafanya ili kuwashirikisha watu uzuri wa imani, uelewa wao kuhusu Mungu na kuzipeleka roho kwa Mungu. Utume mkubwa kabisa wa waumini wa Prelature ni ule wanaoubeba katika mazingira yao ya kila siku, sio kama juhudi za kikundi, bali kama maisha ya kawaida na wajibu wao wa Kikristo. Utume huu unashuhudia urafiki kama tunu ya kweli ya Kikristo; Mkristo mzuri hujitahidi kuwa mwaminifu na rafiki wa kweli. Aidha, kutokana na hamasa waliyo nayo ya kuchangia kuleta ubora wa dunia na kuwasaidia wenye uhitaji mkubwa sana, wanachama wa Opus Dei wanaungana na wengine kuandaa miradi ya elimu na ya kijamii (k.m. shule, hospitali, vituo vya kufundisha wataalamu mbalimbali, vyuo vikuu, n.k). Hayo yote ni anuwai na huwa yanaakisi uhalisia wa kila nchi na mila zinazohusika.

Je, Opus Dei inaweka wazi majina ya wanachama wake?

Ingekuwa vigumu Opus Dei kufanya kazi zake iwapo wanachama wanaozisimamia hawangejionesha kuhusika kwao. Hata hivyo, Opus Dei haiwatambulishi majina yao lakini huwaachia wanachama wajitambulishe wenyewe, ikiheshimu uhuru wao kuhusu hilo. Kwa hiyo ingawa, kwa kawaida, wanachama hawajitangazi kwa umma, vilevile hawajifichi. Marafiki, ndugu na jamaa watajua tu.

Nini uhusiano kati ya Opus Dei na Taasisi nyingine za Kanisa?

Prelature ya Opus Dei na yeyote kati ya waamini wake wanajitahidi kushirikiana kidhati na Baba Mtakatifu (Papa), Maaskofu, Mapadre, na vyombo vyote vya kanisa. Muasisi wa Opus Dei alirudia mara nyingi kusema kuwa Opus ipo kutumikia Kanisa na kwamba wafuasi wa Prelature lazima wawe kichocheo cha umoja.

Je, Opus Dei ina msimamo wake thabiti kisiasa, kiuchumi au kijamii?

Opus Dei haina msimamo binafsi kuhusu siasa, uchumi, wala masuala ya kijamii. Inahimiza uhuru wa kila mtu katika kuyakabili masuala ya sasa. Kama ilivyo kwa Mkatoliki yeyote, wanachama wa Opus Dei wanatakiwa kujifunza kwa undani na kuyafuata mafundisho ya Kanisa kuhusu imani na maadili. Kingine chochote nje ya mtazamo huu, Opus Dei inawaachia uhuru wanachama wake kuwa na misimamo yao.

Nini uhusiano kati ya Opus Dei na Kanisa alipo mwanachama?

Kama sehemu ya Kanisa Katoliki, Opus Dei inafanya kazi kwa karibu sana na Askofu mwenyeji alipo mwanachama. Kibali chake ni muhimu kabla kituo cha Opus Dei kuanzishwa katika Jimbo lake, na daima anapewa taarifa zote kuhusu shughuli za Opus Dei katika Jimbo lake. Uhusiano wa Walei wa Opus Dei na Parokia zao na Askofu wao ni sawa na ule wa Wakatoliki wengine. Kama ilivyo kwa Wakatoliki wengine nao wanabanwa na sheria za Jimbo na wanavyofuata mafundisho na miongozo ya Askofu kulingana na mazingira yao. Wajibu wao kwa Opus Dei unalenga maeneo, kama maendeleo ya kiroho na kutimiza wajibu wa utume, ambamo wanachama wanaruhusiwa kufuata njia yoyote ya utakatifu wanayoipenda.

Ofisi za Utume wa Opus Dei katika Afrika Mashariki

Shughuli ya kwanza ya Opus Dei katika Afrika Mashariki ilikuwa ni uanzishaji wa Chuo cha Strathmore cha mataifa mchanganyiko kwa Kidato cha tano na sita kwa wanaume, mwaka 1961. Baadaye Chuo kilijipanua na kuwa Shule ya Strathmore (1977 Sekondari, 1987 Shule ya Msingi) na Chuo Kikuu cha Strathmore (2002).

Aidha mwaka 1961 akina mama wa Opus Dei walianzisha Chuo cha Kianda, Kenya, kilichokuwa kikifundisha uhazili kwa wahitimu wanawake, na Chuo cha Kibondeni kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Utawala kwa wahitimu mbalimbali. Chuo cha Kianda kilifunguliwa mwaka 1977.

Nchini Kenya kuna Club za Vijana kama vile Faida na Hodari. Vyuo vya mafunzo na makazi kama Keri, Satima, Riverside, Mbagathi na Fanusi; na nchini Uganda kuna Teemba na Bugala zinazoendesha shughuli katika fani za uweledi, mila na kiroho kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu na Vyuo vinginevyo.

Mchanganyiko wa kozi kwa watu mbalimbali, mathalani mafungo, yinaendeshwa mara nyingi kwenye vituo vya Mikutano kama vile Tigoni, Jahazi na Tusimba (Uganda). Aidha huko Tigoni, Kimlea Girls Technical Training Centre kinaendesha kozi katika kilimo, ushoni, kudarizi, na upishi; huko Vipingo, Tewa Training Centre inatoa mafunzo ya uongozi wa taasisi; na Pearlcrest School of Hospitality and Management iliyopo Uganda hufundisha wanawake masuala ya utalii na ukarimu.

Kuna shughuli vilevile katika miji ya Kenya, Kampala, Dar es Salaam na Kigali. Safari nyingi za kutembelea huko huwa zinafanywa.

Kwa Taarifa zaidi wasiliana na:

Opus Dei Information Office, P.O. Box 19884,00100 GPO Nairobi; Tel: +254 020 2151158

Email: info@opusdei.or.ke * website: www.opusdei.or.ke