St. Josemaria Prayercard - Kiswahili

St. Josemaria Prayercard - Kiswahili

Ee Mungu, kwa maombezi ya Bikira Maria Mtakatifu, ulimjalia padri wako Mtakatifu Josemaría neema nyingi zisizohesabika, ukamchagua kuwa mtume wako mwaminifu kupindukia ili aanzishe Opus Dei, njia ya kujitakasa katika kazi za kila siku na katika kutimiza wajibu wa kawaida wa Mkristu. Nisaidie mimi pia ili nami niweze kuyafanya mambo yote ya maisha yangu yawe nafasi ya kukupenda na kulitumikia Kanisa, Baba Mtakatifu na watu wote kwa furaha na moyo mwepesi, nikiangaza njia zote duniani kwa mwanga wa imani na upendo. Kwa maombezi yake Mtakatifu Josemaría, nijalie msaada ninaokuomba .... (taja ombi lako hapa). Amina. Baba yetu. Salamu Maria. Atukuzwe Baba.


Download St. Josemaría Prayercard - Swahili