Rekodi za vipindi vya sala katika mfungo mrefu

Mfungo mrefu ama spiritual retreat - zile siku chache zinazoekwa kando kila mwaka kwa ukimya na maombi - umekuwa mila dhabiti tangu enzi za Bibilia.

Lengo la mfungo kama huu ni kutafakari kwa undani maendeleo yetu ya kiroho, na kufikiria juu ya mapenzi yake mwenyenzi Mungu kwetu, na vile mambo haya yanavyotuongoza katika maisha yetu na katika uhusiano wetu na jirani zetu.

Kwenye kiungo hiki, utapata rekodi kumi za vipindi vya maombi katika mfungo mrefu mmoja ikiongozwa na padre wa Opus Dei.